Wadudu wajulikanao kama senene ni kitafunwa kitamu cha kipekee katika jamii nyingi nchini Uganda na mataifa jirani kama Tanzani na Rwanda.
Lakini wadudu hao wameanza kuwa adimu katika maeneo ambako wamekuwa wakipatikana kwa wingi, hususan kusini mwa Uganda sehemu za Masaka.
Hali hii inaelezwa kusababishwa na uharibifu wa mazingira hususan kutoweka kwa misitu ikihusiana na ukataji miti.
Senene wanapatikana misimu miwili nchini Uganda na ni kitega uchumi kikubwa kwa wafanyabiashara ndogondogo.
Video: Isaac Mumena
#senene #vyakulaasili #uganda #wadudu