Duration 5:14

MRADI WA TIMCI WA KUTAMBUA MAGONJWA MAKALI KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 5 WATUA TANGA JIJI

130 watched
0
0
Published 11 Jun 2021

Katika kuhakikisha vifo vya watoto chini ya miaka mitano vinapungua serikali imetunga sera ya matibabu bure ili kuhakikisha inatokomeza vifo hivyo huku ikisisitiza kuwa utekelezaji wa sera hiyo ni wajibu wa kila mtu ili kuzuia vifo ambavyo vingeweza kuepukika Hayo yamebainishwa na katibu tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Hassan wakati wa uzinduzi wa mradi wa TIMCI katika Jiji la Tanga wenye lengo la kuwawezesha watoa huduma wa afya kutoa huduma stahiki za uchunguzi na utambuzi wa magonjwa ya watoto chini ya miaka 5 kwa kutumia vifaa tiba vya kupimia oksjeni mwilini na vifaa visaidizi vya matumizi ya kielekroniki Awali katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Hassan ameeleza takwimu za vifo vya watoto chini ya miaka mitano na kubainisha kuwa bado hali hairidhishi kutokana na takwimu za vifo vya watoto hao za mwezi Januari hadi Machi 2021 zinazoeleza kuwa watoto waliofia tumboni ni 64, watoto waliofariki mara baada ya kuzaliwa ni 65, vichanga kuanzia siku 0 hadi 28 ni watoto 53 kati ya watoto 1000 waliozaliwa, na chini ya miaka mitano ni watoto 35

Category

Show more

Comments - 0