Duration 3:22

Historia ya Aslay Kabla hajakuwa maarufu - nichombeze

118 184 watched
0
425
Published 24 Oct 2018

Historia ya Aslay Kabla hajakuwa maarufu Isihaka Nassoro au maarufu kama Dogo Aslay (alizaliwa 6 Mei, 1995) ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania. Alianza kufahamika kuanzia mwaka 2011 baada ya kutoa kibao chake cha Nakusemea alichokitoa akiwa chini ya Mkubwa Fella. Kabla ya hapo, alitoa wimbo mwingine uitwao Niwe Nawe akiwa amemshirikisha Temba. Baadaye akatoa nyimbo nyingine kadhaa kabla ya kujiunga na bendi ya vijana ya Yamoto Band. Akiwa ndani ya bendi hiyo, alionesha uwezo mkubwa wa kuimba, akiwa na wenzake, Beka Flavour, Maromboso na Enock Bella. Nyimbo alizoshiriki kutunga na kuimba akiwa Yamoto Band ni pamoja na Yamoto (Nitajuta), Cheza Kwa Madoido, Mama, Nisambazie Raha na nyingine nyingi. Yamoto Band haikudumu sana ambapo ilianza 2013/2014 hadi 2017 ilipovunjika kwa sababu mbalimbali na wasanii waliokuwa kwenye kundi hilo kuanza kufanya kazi zao kwa kujitegemea. Kuanzia 2017, Aslay akiwa msanii wa kujitegemea chini ya meneja wake wa zamani, Chambuso, alianza upya kung'ara.[1] Akiwa msanii wa kujitegemea, ametoa nyimbo nyingi mfululizo hali ambayo imechanganya wengi, lakini mwenye alielezea kwanini amefanya ni kwa sababu hana nyimbo nyingi alizofanya akiwa msanii wa kujitegemea zaidi ya zile alizokuwa na Yamoto Band. Ili asiimbe za Yamoto akiwa kwenye matamasha, kaamua kutoa nyimbo nyingi. Nyimbo hizo ni pamoja na Angekuona, Usiitie Doa akiwa na Khadija Kopa, Muhudumu, Baby, Likizo, Pusha Natamba na Huna. Awali ilitazamika kama Mkubwa Fella ndiye hasa mmiliki wa muziki wa kizazi kipya, lakini kupitia Aslay, Chambuso anasema si lazima yeye ndiye awe meneja bora wa muziki huu.

Category

Show more

Comments - 34