Duration 15:36

Salama Na CPWAA Ep 29 | KILA CHOMBO NA WIMBILE Part 2

25 290 watched
0
258
Published 15 Aug 2020

#YAHStoneTown #SalamaNa #PodCast SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs Listen our Podcast on Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm� �� ‪ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru� �� GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack ‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa Wakati Parklane iko juu sana wengi wetu tulikua tunamfahamu zaidi Sumalee na ilikua haswa Sumalee na yule mwengine mwenye sauti nzito ambaye alikua anatupia tu vichombezo vya hapa na pale, hata kwenye posters za show na mambo mengine Ismail Sadiq aka Sumalee ndo alikua kila kitu mpaka pale kundi lilipovunjika na kila mmoja akaenda upande wake, hapo ndio tulipoanza kufaidi kipaji cha huyu mwanachama mwengine wa hiyo duo, jina la serikali ni Ilunga Khalifa aka Cpwaa alianza kung’ara zaidi na kupata mpaka show za kimataifa. Yuko na swagg, anaweza kuongea kiswahili na kizungu kwa ufasaha na vile vile yeye ndo mfalme wa crank music hapa nyumbani Tanzania. Nani ambaye hakuzimia style ile ambayo Cpwaa alikuja nayo? Nani ambaye hakushangaa alipoona kipaji chake kama solo artist kipindi kile? Maana ki ukweli yeye alikua wa juu kwa juu tu kwenye kundi na zaidi mwenzake ndo alikua anafahamika zaidi? Alitushangaza sote na pia tulimpoke kwa mikono miwili. Kama mwanafunzi Ilunga alikua ni mtu wa kupasi kwa maksi za juu haswa na nna uhakika kama insengekua mziki kipindi kile (sijaribu kusema kwamba mziki ni kitu kibaya) ila anagezingatia masomo kwa asilimia mia moja basi naamini anagekua mbaaali kuliko alipo sasa (na si kwamba alipo sasa ni pabaya). Akiwa anazunguka kwenye tour yeye na mwanaye Ismail kipindi hicho, Ilunga alikua anakosa sana masomo mpaka kuna kipindi ilikua inabidi atungiwe mtihani mwengine na aufanye peke yake maana wenzake wanakua washafanya mitihani yao wakati yeye alikua nje ya Dar es Salaam kuendeleza kipaji chake na kutoa burudani. Sasa, nini haswa kilotokea kati yake yeye na Ismail? Kwanza haswa walikutana lini? Wapi? Ilikuaje siku ya kwanza? Na kama kundi walikua wanaishi vipi? Waliwezaje ku handle umaarufu kipindi hicho? Walikua wanatengeneza pesa? Je wazazi wake walikua wanamruhusu kukosa shule na kufanya mziki? Nani alimfanya yeye avutiwe na mziki? Ana majuto yoyote katika maisha yake? Na je Baba na Mama yake ni watu wa aina gani? Ameoa? Mtoto? Kazi gani anafanya? Pia alikua rafiki mzuri wa Marehemu Mangwair, kifo chake kimemuathiri vipi? Na industry ya sasa je anaweza kutoboa? Wallahi kulikua na maswali mengi Ila na majibu nayo hayakua nyuma, yangu matumaini na hii pia itakufunza jambo, tafadhali enjoy. Love, Salama. Soundtrack Yeah by @MarcoChali /watch/QLnf4BH1euC1f Follow: Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown

Category

Show more

Comments - 56